Wednesday, 18 March 2015

INTERNAL WALL PAINT FOR AL'MASJID ISLAMIYYA


SWAHILI
Habari! 
Napenda kuwajulisha michango imefika kiasi cha taslim TZS 240,000/=. Ndoo mbili za rangi nyeupe aina ya Coral - Silk zimenunuliwa tayari. Rangi aina hii ni ya kudumu pindi ukuta unapokumbwa na mafuta basi kitambaa chenye maji ya sabuni kidogo tu na kufuta sehemu iliyoingia na mafuta ambayo yamesababishwa na vidole, mikono ama kichwa n.k. Msikiti unabaki umeng'aa vizuri sana na kuonekana mpya kila kukicha.

Nasubiria ahadi zingine mwisho huu wa mwezi ambazo zitamalizia kununua vifaa kadha wa kadha ambavyo vimebaki.

Kwa niaba ya AL'MASJID ISLAMIYYA, Kata ya Kidole - Ukonga tunawashukuru sana kwa michango yenu na Mola awaongezee zaidi na atuwezeshe kufanya wepesi katika kila jambo la kheri tunalolifanya. 

SHUKRAN.



ENGLISH 
Hello! 
I would like to inform you the outstanding balance for the donation is TShs. 240,000/=.









1 comment:

  1. Wish You All The Best ONAG FOUNDATION for the efforts and proud to be your sponsor for this wonderful thing you're doing.

    ReplyDelete